Meles Zenawi ‘anaendelea vizuri’

Image caption Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi

Waziri Mkuu Hali ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi ‘ni nzuri na anapata nafuu", msemaji wa serikali ameiambia BBC, na kufutilia mbali taarifa kuwa anaumwa sana.

Hata hivyo, Bereket Simon amekataa kutoa taarifa zaidi kuhusu aliko Bw Meles' na anachoumwa.

Bw Bereket awali alinukuliwa akisema kuwa Waziri huyo Mkuu mwenye umri wa miaka, 57, alikuwa mapumziko.

Tetesi zilianza wakati aliposhindwa kuhudhuria mkutano wa AU mwezi uliopita.

Kuna taarifa kuwa Bw Meles alikuwa hospitali nchini Ublegij akisumbuliwa na matatizo ya tumbo.

Lakini Bw Bereket alinukuliwa akisema na gazeti la ‘The Reporter’ kuwa vikosi vya upinzani vilikuwa vinajaribu kujenga mazingira kuwa ‘ya kuchanganya’ kwa kusema kwa kuelezea hali ya afya ya waziri huyo mkuu.

Alikiambia kipindi cha BBC Focus on Africa kuwa ‘haikuwa sahihi’ kutoa taarifa zaidi.

Alipoulizwa nani alikuwa anasimamia nchi wakati Bw Meles akitibiwa, alijibu: "Hali iko shwari, hakuna mabadiliko yoyote na hakutakuwa na mabadiliko yoyote kwa siku za karibuni."

Inaaminika kuwa Bw Meles alionekana hadharani mara ya mwisho katika mazungumzo ya G20 nchini Mexico mwezi Juni.

Alichukua madaraka kuongoza vuguvugu la waasi lililoiondoa serikali ya kikomunisti ya Mengistu Haile Mariam mwaka 1991.

Ameshinda uchaguzi mara kadhaa tangu wakati huo lakini wapinzani wake wamekuwa wakimtuhumu kutumia nguvu kubakia madarakani.