Viongozi Somalia wapitisha katiba mpya

Haki miliki ya picha a
Image caption Katiba mpya yapitishwa Somalia

Viongozi wa Somalia wanaokutana Mogadishu kwa wingi wameipitisha katiba mpya ya nchi hiyo hivyo kufungua njia kwa serikali mpya kuchaguliwa mwezi huu.

Kura hiyo imepigwa muda mfupi baada ya watu wawili kujilipua wenyewe nje ya jingo la mkutano.

Chini ya mpango ulioungwa mkono na Umoja wa Mataifa bunge jipya litachagua kiongozi mpya wa Somalia Agosti 20.

Somalia imekuwa katika vita na kundi la al-Shabab kwa miongo miwili na huku kundi hilo likidhibiti maeneo mengi ya nchi.

Serikali yake ya mwisho iliondolewa madarakani mwaka 1991.