Chuo Kikuu cha fungwa Sierra Leone

Image caption Sierra Leone

Chuo Kikuu cha zamani zaidi katika Afrika mangaribi kilicho Sierra Leone kimefungwa kufuatia vurugu za wanafunzi.

Mwandishi wa BBC katika eneo hilo Umaru Fofana anasema zaidi ya wanafunzi 1000 waliteketeza magurudumu makuukuu ya magari na kufunga milango ya majengo yote katika chuo hicho cha Fourah Bay.

Fujo hizo zilitokana na hatua ya wakuu wa shule kuwatimua wanafunzi 13 kwa madai ya kuongoza uvamzi wa bweni moja ambalo limefungwa kwa miaka miwili.

Wanafunzi walifamia chuo hicho wakidai kuwa kufungwa kwake kumefanya maisha kuwa magumu kwa familia zinazotoka jamii maskini.

Wakati wa fujo hilo wanafunzi wengine walikuwa wakifanya mtihani yao na hivyo sasa mitihani hiyo imehairishwa.

Wakuu wa chuo hicho wanakutana kutafuta suluhu la fujo hilo.