Saha aanzisha mazungumzo na Sunderland

Imebadilishwa: 16 Agosti, 2012 - Saa 12:20 GMT
Louis Saha

Louis Saha


Louis Saha amesafiri Kaskazini Mashariki mwa London, kuanzisha mazungumzo na klabu ya Sunderland.

Kwa mujibu wa ripoti aliyochapisha kwa mtandao wa Twitter, Saha, mwenye umri wa miaka 34, ambaye alikihama klabu ya Tottenham mwisho wa msimu uliopita, hajasajiliwa na klabu yoyote.

''Ningependa kuwajulisha kuwa nasafiri kwenda kujadiliana na wasimamizi wa klabu ya Sunderland, kuhusu usajili wangu, na nitawajulisha matokeo yake'' alisema Saha.

Saha alijiunga na klabu ya Tottenham Hotspurs, kwa mkataba wa muda mfupi mwezi Januari kutoka kwa klabu ya Everton, lakini kandarasi yake haikuongezwa baada ya msimu wa ligi ulipomalizika.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.