Bomu laua wawili mjini Tripoli

Imebadilishwa: 19 Agosti, 2012 - Saa 19:37 GMT
Athari ya mlipuko wa bomu mjini Tripoli

Athari ya mlipuko wa bomu mjini Tripoli

Maafisa wa usalama wa Libya wamesema mabomu mawili yaliyokuwa kwenye gari yamelipuka katikati ya mji mkuu wa Tripoli,

moja karibu na ofisi ya wizara ya mambo ya Ndani na jingine karibu na chuo cha kijeshi.

Taarifa zinasema milipuko hiyo imeua watu wawili na kuacha wengine wanne kujeruhiwa katika chuo cha zamani cha kijeshi cha wanawake.

Hili ni shambulio kubwa la kwanza kutokea tangu kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi mwaka jana.

Mkuu wa Usalama wa mji Tripoli amelaani mashambulizi hayo yaliyolengwa kwa watu wanaomuunga mkono rais wa zamani wa nchi hiyo marehemu Mummar Gaddaf.

Katika hosptali ya Al Jalaa iliyopo Tripoli, Wesan Abu Alsoude ambaye binamu yake aliuawa amelaumu mamlaka kwa kushindwa kuchuchukua hatua kuzuia shambulio hilo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.