Sina nia ya rekodi mpya-Bolt

Imebadilishwa: 23 Agosti, 2012 - Saa 12:56 GMT
Usain Bolt

Usain Bolt

Usain Bolt wa Jamaica amesema hana nia yoyote ya kuvunja rekodi ya ulimwengu ya mita Mia Mbili wakati wa mashindao ya Diamond League yatakayofanyika leo usiku katika uwanja wa Pontaise mjini Lausanne.

Bingwa huyo wa Olimpiki anaongoza wanariadha wengine 19 walioshinda medali za dhahabu wakati wa michezo ya Olimpiki mjini London.

Bolt anapambana na Warren Weir, Jason Young na Nickel Ashmeade pamoja na Wallace Spearmon kutoka Marekani katika mbio hizo za mita Mia Mbili.

Bolt anashikilia Rekodi ya Dunia ya mbio hizo kwa mda wa sekunde 19.19 alouweka mwaka wa 2009 wakati wa fainali ya mashindano ya Dunia mjini Berlin.

Katika mbio za mita 100 mshindi wa Medali ya fedha katika michezo ya Olimpiki mjini London naye atakabiliana na Mmarekani Tyson Gay aliyemaliza wa nne pamoja na Ryan Bailey.

Jumla ya wanariadha 52 walioshinda nishani mbali mbali wakati wa michezo ya olimpiki mjini London watashiriki katika awamu hiyo ya 11 ya mashindano ya IAAF Diamond League.

Katika mbio za mita Mia moja kwa kina dada Shelly Ann Fraser-Pryse anamenyana na Carmelita Jeter na Veronica Campbell-Brown.

Mashindano yajayo ya Diamond League yatafanyika mjini Zurich Tarehe 30 Agosti huku awamu ya yakiandaliwa mjini Brussels Ubelgiji September 7.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.