Israel na Afrika Kusini zazozana

Imebadilishwa: 23 Agosti, 2012 - Saa 13:07 GMT
Rais Jacob Zuma

Rais Jacob Zuma

Israili imekasirishwa na uwamuzi wa serikali ya Afrika ya Kusini wa kupiga marufuku nembo zinazowekwa kwenye bidhaa ambazo zina nembo isemayo ''made in Israel'' il hali zimetengenezwa Ufuko wa magharibi.

Badala yake Afrika ya Kusini inataka bidhaa hizo zibainishwe kwa kuandikwa kuwa zimetengezwa katika ''maeneo yanayokaliwa''

Wizara ya mashauri ya nje ya Israil itaja hatua hiyo kama ya ubaguzi.

Makaazi, miji ya Israili iliyojengwa katika maeneo yanayozozaniwa ya wa Palestina ni kinyume cha sheria ya Kimataifa ingawa Israili inapinga hilo.

Afrika ya Kusini inaaminika kuwa nchi ya kwanza kujaribu kutimiza uamuzi huu kisheria ingawa serikali nyingine kama Uingereza, zimewahi kuyashauri maduka makubwa yabainishe bidhaa zitokazo kwenye makaazi ya walowezi wa Israili.

Lakini kuanzia leo nchini Afrika ya Kusini, bidhaa kutoka makaazi hayo ya Israili, hazitokubalika kuwa na nembo "made in Israel".

Wizara ya mashauri ya nje ya Israili, imeutaja uwamuzi huo kama wa Ubaguzi wa rangi na usiokubalika.

Wizara hiyo imemtaka Balozi wa Afrika ya kusini nchini Israili aeleze hatua ya serikali yake.

Kuna kampeni inayofanywa miongoni mwa wa Palestina na waungaji mkono wao ya kususia bidhaa zinazotengenezwa ndani ya maeneo yanayokaliwa na walowezi wa Kiyahudi pamoja na Israili kwa ujumla.

Msemaji wa vuguvugu la Afrika ya Kusini ameutaja uamuzi wa Afrika ya Kusini kama ishara tu lakini akaonyesha matumaini utakua chachu kwa wengine.

Raia wa Palestina wanaopendelea vikwazo mara kwa mara hutumia mfano wa juhudi za uhuru huko Afrika ya Kusini kama changamoto na kuishutumu Israili kuwa inaendesha sera ya ubaguzi na kuongoza dola la kiimla, Israili inapinga tuhuma hizo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.