West Ham kumsajili Jarvis

Imebadilishwa: 23 Agosti, 2012 - Saa 10:22 GMT
Wachezaji wa Wolves

West Ham imeafikia mkataba ambao unakisiwa kugharimu kitita cha pauni milioni Kumi nukta Saba Tano kumsajili mcheza kiungo wa Wolverhampton Matt Jarvis.

Mkataba huo uliafikiwa na vilabu hivyo siku ya Jumatano na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, anatarajiwa kusafiri hadi London ili kujadiliana na klabu hiyo kuhusu malipo yake, kabla ya kufanyika kwa uchunguzi wa kimatibabu.

West Ham italipa pauni milioni Saba Nukta Tano kama malipo ya mwanzo na kulipa masalio kwa muda.

Klabu ya Sunderland vile vile imeripotiwa kutaka kumsajili Jarvis, lakini haijawasilisha ombi lolote rasmi.

Kocha wa West Ham Sam Allardyce amekuwa akifuatilia hali ya mchezaji huyo kwa muda na anatarajiwa usajili wa mchezaji huyo utakamilika kabla ya mechi yao siku ya jumamosi dhidi ya Swansea.

Jarvis, ambaye ameichezea timu ya taifa ya England mechi mocha, aliichezea klabu ya Wolverhampton siku ya Jumanne wakati ilipoilaza Bransley kwa mabao Matatu kwa Moja.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.