Kiboko afa bwawani

Imebadilishwa: 24 Agosti, 2012 - Saa 17:34 GMT

Kiboko aliyepotea njia na kuingia kwenye bwawa la kuogelea nchini Afrika Kusini, amenasa na kufa.

Kiboko akiwa kwenye bwawa

Walinzi wa mbugani na wataalamu wengine walitoa maji kwenye bwawa hilo, na wakipanga kumpa nus-kaput kiboko huyo na kumuondoa kwa winchi, lakini alifariki kabla ya kuokolewa.

Awali juma hili, kiboko huyo alitoroka kundi lake katika mbuga ya kibinafsi ya wanyama pori, kaskazini mwa Afrika Kusini, na kuingia kwenye bwawa la nyumba ya mbuga hiyo.

Bwawa hilo halikuwa na ngazi, na hakuweza kutoka mwenyewe.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.