Wachimba migodi waanza kurudi kazini

Imebadilishwa: 25 Agosti, 2012 - Saa 15:19 GMT

Kampuni ya migodi iliyokuwa chanzo cha mgomo wa ghasia Afrika Kusini, Lonmin, inasema kuwa wafanyakazi wake zaidi wamerudi kwenye mgodi wa Marikana, karibu na Rustenberg.

Polisi nje ya mgodi wa Marikana wakati wa mgomo

Juma lilopita wachimba migodi 34 waliogoma walipigwa risasi na polisi na kuuwawa, na kama 70 walijeruhiwa.

Serikali ya Afrika Kusini imeteua tume ya majaji kuchunguza kilichotokea.

Lonmin inasema kuwa katika mgodi wa Eastern Shafts, huko Marikana, 57% ya wachimba migodi wako kazini Jumamosi.

Sehemu nyengine ya machimbo imefungwa kwa sababu ya mapumziko ya mwisho wa juma.

Kampuni inasema hali ni ya amani, na kwamba mazungumzo yanaendelea ili kushawishi wafanyakazi wote warudi kazini.

Lakini uchimbaji wa madini ya dhahabu nyeupe, platinum, ulisimamishwa kwenye mgodi huo zaidi ya majuma mawili yaliyopita kwa sababu ya mgomo, na bado kazi haikuanza.

Mazishi ya baadhi ya wachimba migodi waliokufa yamefanywa na mawaziri walihudhuria na kuahidi kuzisaidia familia za wachimba migodi hao.

Wakuu sasa wamethibitisha kuwa kati ya waliokufa, watano walikuwa wageni kutoka nchi za nje.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.