Waziri mkuu wa zamani Somalia kutoa fidia

Imebadilishwa: 29 Agosti, 2012 - Saa 11:45 GMT

Mohammed Ali Samantar

Aliyekuwa Waziri mkuu wa Somalia, Mohamed Ali Samantar, amekubali kuwalipa dola millioni ishirini na moja waathirika wa mateso yaliyotendeka wakati alipokuwa mamlakani katika miaka ya themanini.

Haya yamejitokeza katika kesi iliyofuatiliwa kwa karibu sana na wanaharakati wa haki za binaadam na ambayo iliwasilishwa nchini Marekani na wasomali saba.

Hata hivyo bwana Samantar, ambaye sasa anaishi katika jimbo la Virginia, nchini Marekani amakanusha madai ya kuamuru mateso hayo.

Alisimamisha kesi yake baada ya kuambaia mahakama kuwa amefilisika.

Waathrika walidai kuwa vitendo vya mauaji , ubakaji na mateso dhidi ya waathirika, vilifanywa na maafisa wa ujasusi wa Somalia kwa ushirikiano na polisi wakati Samantar alikuwa waziri mkuu kuanzia mwaka 1987 hadi mwaka 1990.

Lakini Samantar alijitetea akisema kesi hiyo ilishinikizwa kisiasa na kwamba itasababisha mgawanyiko zaidinchini Somalia ambayo bado inakabiliwa na mapigano.

Alisema ''Nilifanya kazi kwa miaka 40 nchini Somalia. Nilijitolea kuihudumia nchi yangu na vile vile nilitii sheria.''

Kesi hiyo ambayo lengo lake lilikuwa kuwalipa fidia waathirika kwanza ilitupiliwa mbali na jaji mmoja ingawa baadaye ilianza kusikilizwa tena na mahakama ya rufaa.

Mnamo mwaka 2010, mahakama ya juu zaidi iliamua kuwa bwana Samantar hangeweza kulindwa na sheria za kidiplomasia.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.