Tutu asema Blair na Bush walikosa

Imebadilishwa: 2 Septemba, 2012 - Saa 18:32 GMT
Askofu Desmond Tutu

Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini, ambaye kwa miaka mingi alipinga ubaguzi wa rangi nchini mwake, amezusha tena swala la vita vya Iraq.

Anataka waziri mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair, na rais wa Marekani wakati huo, George Bush, washtakiwe kwa mchango wao katika vita hivo.

Akiandika kwenye gazeti la Uingereza la Observer, Askofu Tutu amesema viongozi hao wawili walisema uongo kwamba Iraq ilikuwa na silaha za maangamizi makubwa; na hivo wanafaa kufikishwa mbele ya Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, ICC, kuwajibika kwa vifo vya watu wengi katika vita hivo.

Alisema uvamizi wa Iraq umetibua utulivu katika dunia, na kupelekea vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Syria.

Tony Blair ameyatoa maanani maneno hayo kwamba hayana msingi na kwamba siyo mepya.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.