Walimu Kenya waanza mgomo

Imebadilishwa: 3 Septemba, 2012 - Saa 13:01 GMT

wanafunzi wakiwa darasani kabla ya mgomo

Maelfu ya walimu nchini Kenya wameanza mgomo wakidai maslahi zaidi, ambao umeathiri shule nyingi za msingi nchini humo.

Walimu hao wamedharau amri ya mahakama ambayo ilibatilisha mgomo huo kwamba sio halali.

Shule nyingi zilizotembelewa na waandishi wa BBC Nairobi na Mombasa zilikuwa zimefungwa.

Walimu wanataka mshahara uongezwe kwa asilimia 100 na 300%.

Walimu wa shule za sekondari na wale wa vyuo vikuu wamesema watajiunga katika mgomo huo baadae wiki hii, wakati vyuo vyao vitakapofunguliwa kwa muhula mpya.

Hadi sasa serikali bado haijazungumza lolote kuhusu mgomo huo.

Mhariri wa BBC Idhaa ya Kiswahili Afrika Mashariki David Okwemba amesema mgomo huo unaonekana kushika kasi.

Katika jiji la Nairobi waalimu wamebeba mabango baadhi yao limeandikwa " Waalimu hatuwezi kula panya na tumechoka na ahadi zisizotekelezeka.

Mgomo huo wa waaalimu umeitishwa na chama cha waalimu unaowawakilisha 250,000.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.