Ethiopia yazungumza na kundi la Ogaden

Imebadilishwa: 9 Septemba, 2012 - Saa 10:02 GMT
Wapiganaji wa Ogaden

Mazungumzo ya amani yamefanywa baina ya serikali ya Ethiopia na wapiganaji wa Ogaden, ONLF, chama ambacho kimekuwa kikipigania kulitenga eneo la magharibi mwa Ethiopia kwa karibu miongo mitatu.

Mazungumzo hayo yaliyofanywa Nairobi awali juma hili, yaliandaliwa na serikali ya Kenya.

Kundi la ONLF limefanya mashambulio kadha katika miaka ya karibuni, moja dhidi ya mtambo wa kuweka gesi mwaka wa 2007 ambalo liliuwa Waethiopia kadha na wafanyakazi tisa kutoka Uchina.

Watu wengi wa eneo la Ogaden la Ethiopia ni wa asili ya Kisomali.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.