Serikali ya Sri Lanka yashinda Tamil

Imebadilishwa: 9 Septemba, 2012 - Saa 15:26 GMT
Rais Mahinda Rajapaksa wa Sri lanka alipozuru Uingereza mwezi wa Agosti

Serikali ya mseto ya Sri Lanka imeshinda kwa kiwango kidogo katika uchaguzi wa serikali za mitaa mashariki mwa nchi, eneo ambalo liliharibika sana wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka mingi.

Ingawa chama kikuu cha Watamil kilipata kura karibu sawa na serikali, hata hivo kimechukua nafasi ya pili katika jimbo hilo ambako jamii za Watamil, Waislamu na Wasinhala ziko karibu sawa.

Mwandishi wa BBC mjini Colombo anasema Rais Mahinda Rajapaksa atatosheka kuwa serikali yake ya mseto angalau bado inaongoza katika jimbo ambako vita na wapiganaji wa Tamil Tigers vilimalizika miaka mitano iliyopita.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.