Wabunge wa Somalia waanza kumchagua rais Mpya

Imebadilishwa: 10 Septemba, 2012 - Saa 14:01 GMT

Uchaguzi Somalia

Wabunge 257 wa bunge jipya la somalia wanapiga kura wakati huu kumchagua rais mpya wa taifa hilo.

Shughuli ya upigaji kura ilichelewa kwa sababu kikosi cha umoja wa mataifa kilikuwa kinawachunguza wabunge katika ukumbi wa zoezi hilo..

Wagombea ishirini na wanne wanawania urais akiwemo rais anayeondoka Sheikh Sharif Sheikh Ahmed na waziri mkuu Abdiweli Mohamed.

Kamati ya uchaguzi imeidhinisha idadi ya wagombea 25 wa kiti hicho , akiwemo rais wa serikali ya mpito Sheikh Sharif sheikh Hassan na waziri mkuu Abdiweli Mohamed Ali.

Serikali ya mpito ambayo imedumu kwa muda wa miaka minane itakabidhi mamlaka kwa serikali mpya baada ya uchaguzi wa rais.

Rais wengi wa Somalia walilazimika kuikimbia nchi yao kufuatia hali mbaya ya usalama nchini Mwao.

Baadhi yao wanaoishi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya wamekuwa na hisia mbali mbali kuhusu na mchakato wa kuleta amani na usalama pamoja na uthabiti unaoendelea nchini Somalia.

Mwandishi wa BBC mjini humo Daud Aweis anasema kuwa shughuli itachelewa kuhu wabunge wakipitia ukaguzi mkali kuhakikisha usalama wakati wa uchaguzi huo.

Ni Mara ya kwanza kwa miaka mingi kwa rais kuchaguliwa nchini Somalia ikiwa ni ishara ya usalama kuimarika.

Hata hivyo kundi la wapiganaji la al-Shabab, bado linadhibiti maeneo mengi ya kusini na katikati mwa Somalia.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.