Onyo la WHO na vifo 31 kutokana na Ebola DRC

Imebadilishwa: 13 Septemba, 2012 - Saa 16:11 GMT

Virusi vya Ebola

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mlipuko wa homa ya Ebola, katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imefika watu 31 hadi kufikia sasa na hata inatishia kuathiri miji kadhaa.

Hili ndilo onyo limetolewa na shirika la afya duniani WHO.

Mipuko wa kwanza wa homa hiyo uliripotiwa tarehe kumi na saba mwezi wa saba katika mkoa wa Kaskazini Mashariki wa Orientale.

Afisaa mmoja wa shirika hilo Eugene Kabambi aliambia shirika la habari la Reuters kuwa hali ni mbaya sana na kwamba bado haijadhibitiwa.

Ni rahisi sana kuambukizana homa ya Ebola na homa hiyo huuwa asilimia tisini ya watu ambao huambukizwa.

Hakuna tiba inayojulikana kwa homa hiyo wala chanjo. Homa hiyo husambaa kwa kugusana na husababisha mgonjwa kuvuja sana damu.

Idadi ya vifo vilivyotokana na homa yenyewe katika miji ya Isoro na Viadana, imeongezeka maradufu kwa zaidi ya wiki moja hadi watu 31.

Homa ya Ebola

Inaarifiwa wauguzi watano wamefariki kutokana na homa hiyo.

"homa hii bado haijadhibitiwa. Badala yake hali ni mbaya zaidi hata kuliko awali. Ni mbaya sana'' alisema bwana Kabambi.

"ikiwa hakuna hatua zitachukuliwa sasa hivi, homa hiyo itasambaa hadi maeneo mengine na hata katika miji mikuu,'' aliongeza Bwana Kabamba.

Mwezi jana mlipuko wa aina mbaya sana ya homa hiyo katika nchi jirani ya Uganda ilisababisha vifo vya watu 16 lakini wafanyakazi wa afya wanasema kuwa milipuko hiyo miwili haina uhusiano wowote.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.