Maandamano yasambaa hadi Sudan

Imebadilishwa: 14 Septemba, 2012 - Saa 16:04 GMT

Waandamanaji Sudan

Waandamanaji walioghadhabishwa na filamu inayodhihaki dini ya kiisilamu wameshambulia balozi za Uingereza na Ujerumani mjini Khartoum, Sudan.

Waandamanaji walianza kuwasha moto na kisha kuichanachana bendera ya Ujerumani na kuweka bango lenye maandiko ya kiisilamu ambapo bendera hiyo ilikuwa.

Maandamanao yangali yanaendelea katika nchi za Mashariki ya kati na Kaskazini mwa Afrika kuilaani filamu ya Marekani inayokejeli Mtume Muhammad.

Mjini Cairo, polisi waliwarushia gesi ya kutoa machozi na kuwatawanya waandamanaji takriban 500,kutoka katika ubalozi wa Marekani.

Maandamano pia yalifanyika katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa.

Msemaji wa ubalozi wa Uingereza amethibitisha BBC kuwa maandamano yanafanyika nje ya ubalozi wa Uingereza na kusema kuwa polisi wa Sudan wako katika eneo hilo kudhibiti hali.

Hata hivyo, msemaji huyo hangeweza kuthibitisha ikiwa waandamanaji waliingia katika ubalozi huo au ikiwa maandanamo yana uhusiano wowote na filamu hiyo inayopingwa na waisilamu kote duniani.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.