Viongozi wa Sudan waombwa wakubaliane

Imebadilishwa: 22 Septemba, 2012 - Saa 15:22 GMT

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki-Moon ametoa wito kwa viongozi wa Sudan na Sudan Kusini wafikie makubaliano kamili watapokutana kesho mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na Omar al-Bashir wa Sudan

Bwana Ban alisema marais hao wanafaa kusahau tofauti zao kuhusu mafuta na mipaka, na badala yake wafungue ukurasa mpya wa amani na ushirikiano.

Sudan na Sudan Kusini zilikaribia kupigana vita kamili baada ya mapambano baina ya majeshi yao, kufuatia Sudan Kusini kujitenga na kupata uhuru Julai mwaka jana.

Mazungumzo ya kina yamekuwa yakifanywa, yakisimamiwa na Umoja wa Afrika.

Sudan Kusini imethibitisha kuwa Rais Salva Kiir atakutana na Rais Omar al-Bashir wa Sudan, kwa mazungumzo hapo kesho.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.