Libya yaondosha makundi ya wapiganaji

Imebadilishwa: 23 Septemba, 2012 - Saa 17:00 GMT

Kiongozi wa bunge la Libya amesema kuwa makundi yote ya wapiganaji yasiyokuwa halali yataondoshwa baada ya balozi wa Marekani kuuliwa na moja kati ya makundi hayo juma lilopita.

Mohammed Magarief - kushoto - akipewa hongera alipochaguliwa kuwa rais wa bunge

Hapo jana kundi la wapiganaji lilokuwa na nguvu, mashariki mwa Libya, lilisema kuwa linamaliza shughuli zake.

Pamekuwa na wasiwasi ndani na nje ya nchi, kuwa makundi mengi ya wapiganaji bado yana nguvu - makundi yaliyojitokeza wakati wa vita vya kumuondoa Kanali Gaddafi.

Mkuu wa bunge la taifa, Mohammed Magarief, amesema kuwa makambi na wapiganaji wote wasiodhibitiwa na serikali, yatafutwa:

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.