Rais wa Misri aelekea Marekani

Imebadilishwa: 23 Septemba, 2012 - Saa 16:48 GMT

Rais Mohammed Morsi wa Misri ameisihi serikali ya Marekani kubadilisha msimamo wake sana katika uhusiano wake na nchi za Kiarabu.

Rais Mohammed Morsi

Akizungumza na gazeti la New York Times, kabla ya ziara yake ya kwanza nchini Marekani tangu kuwa rais, Rais Morsi alisema kuwa Marekani inahitaji kuonesha heshima zaidi kwa historia na utamaduni wa nchi za Kiarabu hata kama unagongana na utamaduni wa mataifa ya Magharibi.

Bwana Morsi - ambaye anatoka chama cha Muslim Brotherhood - piya alitoa maanani malalamiko kutoka wakuu wa Marekani kwamba alichukua muda kulaani maandamano dhidi ya Marekani, yaliyozushwa na filamu iliyokejeli Uislamu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.