Viongozi wa Sudan wakutana Ethiopia

Imebadilishwa: 23 Septemba, 2012 - Saa 17:16 GMT

Marais wa Sudan na Sudan Kusini wanakutana katika nchi ya jirani, Ethiopia.

Rais Omar al_bashir (kati) na Rais salva Kiir (kulia)

Umoja wa Mataifa umeongoza wito kwa viongozi hao kutia saini mkataba kamili wa amani.

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini aliliambia shirika la habari la taifa kwamba anatumai kutakuwa na sherehe baada ya mkutano wake na rais wa Sudan, Omar el Bashir.

Wajumbe kwenye mazungumzo ya kupatanisha wanasema wamepiga hatua juu ya maswala kadha kabla ya viongozi hao kuwasili, lakini kuna mengine kadha yaliyosalia.

Maswala ya kujadiliwa ni kuwa na eneo baina ya nchi mbili hizo lisiloruhusu shughuli za kijeshi, kuamua mpaka hasa unapita wapi, mafuta na eneo lenye mzozo la Abyei.

Lengo la mkutano ni kupata suluhu kamili juu ya maswala yote hayo magumu.

Pengine haitawezekana.

Lakini nchi zote mbili zinachagizwa kufikia mapatano.

Umoja wa Mataifa umetishia kuziwekea nchi hizo vikwazo endapo zitaendelea kuzozana.

Na makubaliano yakipatikana, yatasaidia uchumi wa nchi zote mbili.

Sudan Kusini iliacha kuchimba mafuta mwezi wa January kwa sababu ikizozana na Sudan kuhusu ujira inafaa kuilipa Sudan kwa kutumia miundo mbinu ya Sudan wakati wa kusafirisha mafuta yake.

Tangu wakati huo nchi zote mbili zimekuwa na shida za kiuchumi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.