Ehud Olmert hatiani kwa kukiuka sheria

Imebadilishwa: 24 Septemba, 2012 - Saa 13:06 GMT

Ehud Olmert alikumbwa na kashfa nyingi za ufisadi wakati wa utawala wake wa miaka mitatu

Waziri mkuu wa zamani nchini Israel, Ehud Olmert ametozwa faini ya dola 19,170 na kupewa kifungo cha nje cha mwaka mmoja kwa kukiuka sheria.

Olmert alipatikana na hatia ya kumfanyia upendeleo kinyume na sheria mfanyabiashara mmoja wakati alipokuwa waziri.

Hata hivyo kesi ya rushwa dhidi yake ambayo ilimsababisha kujiuzulu mnamo mwaka 2009 ilitupiliwa mbali

Olmert sasa anaweza kugombea ubunge ingawa bado hawezi kuteuliwa kama waziri kwa sababu anakabiliwa na kesi nyingine ya rushwa .

Maafisa mjini Jerusalem wanadaiwa kula rushwa wakati Olmert alipokuwa meya kati ya mwaka 1993 na 2003, na kwa maagizo ya mrithi wake alitakiwa kuharakisha kile kilichojulikana kama ujenzi wa makaazi ya walawezi ya Holyland.

Olmert hata hivyo amekanusha kuwahi kuhusika na kashfa hiyo ya mamilioni ya dola

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.