Mkutano maalum kuhusu Mali New York

Imebadilishwa: 27 Septemba, 2012 - Saa 13:54 GMT

Waasi wa Tuareg nchini Mali

Waziri Mkuu wa Mali ameomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha mpango wa kurudisha udhibiti wa kaskazini mwa nchi kwa serikali kutoka kwa waasi wa kiislamu waliouteka mapema mwaka huu.

Sheikh Modibo Diarra alikuwa akizungumza katika mkutano kuhsu Mali uliohudhuriwa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hilary Clinton,rais wa Nigeria na viongozi wengine wa dunia katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, aliambia mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa, Jumanne, kuwa Ufaransa iko tayari kuunga mkono juhudi za kuirejeshea Mali hadhi yake kama nchi huru.

Jeshi la pamoja la nchi za Magharibi mwa Afrika lijulikanalo kama ECOMOG, na ambalo limewahi kuingilia kati mizozo katika baadhi ya nchi za Afrika, linasema kuwa takriban wanajeshi elfu tatu, wana kibarua cha kutwaa eneo la Kaskazini kutoka kwa wapiganaji hao.

Lakini mwandishi wa BBC anasema kuwa viongozi wa Afrika wanatafuta uungwaji mkono kutoka kwa Baraza la usalama la umoja wa mataifa kabla ya kupeleka wanajeshi huko.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.