Uchunguzi wa mauaji ya Tana waanza

Imebadilishwa: 1 Oktoba, 2012 - Saa 14:13 GMT

Ghasia za Tana zilisababisha vifo vya zaidi ya watu 50

Tume ya mahakama iliyoundwa kuchunguza mauaji ya yaliyotokea Tana River imeanza kazi yake leo huku serikali ikiahidi kuiunga mkono na kusema kuwa wale watakaopatikana na hatia lazima watachukuliwa hatua.

Tume hiyo yenye maafisa saba wa mahakama ilianza kwa kutembelea eneo ambako ghasia zilitokea ili kueleza wananchi kazi yao na majukumu yao katika kuhakikisha haki imetendeka.

Tume hiyo pia imewataka wenyeji wa Tana kushirikiana nayo kwa kutoa habari kuhusu mauaji yaliyotokea kufuatia mapigano kati ya jamii za Pokomo na Orma.

Mwanasheria mkuu Githu Muigai alielezea matumaini kuwa kazi ya tume hiyo, itakuwa ni kupendekeza hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya wale waliohusika na ghasia hizo.

Aidha tume hiyo pia ina jukumu la kutoa mapendekezo ya kuzuia matukio kama hayo katika siku za usoni hasa wakati huu Kenya inapojiandaa kwa uchaguzi mkuu mwezi Machi mwaka ujao.

Wanachama wa tume hiyo ni pamoja na jaji Grace Nzioka, hakimu mkuu Emily Ominde, hakimu Abdulqadir Lorot Ramadhan, bwana Macdonald Oguya na Joseph Narangwi.

Hali iligeuka na kuwa karaha kwa wenyeji wa Tana river pale ambapo jamii za Pokomo na Orma zilifanya mashambulzi la kulipiza kisasi.

Watu 52 waliuawa katika vijiji kvya Riketa huku mauaji mengine ya watu 14 yakitokea katika kijiji cha Chamwanamuma ambako watu 38 zaidi waliuawa ikiwemo polisi tiSA pwani mwa Kenya.

Naibu waziri wa mifugo ambaye pia ni mbunge wa Galole, Dhadho Godhana, alifikishwa mahakamani kwa madai ya uchochezi hali ilyosababisha mapigano kati ya jamii hizo mbili.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.