Wateta kuhusu kesi ya utovu wa nidhamu

Imebadilishwa: 2 Oktoba, 2012 - Saa 14:11 GMT

Maandamano ya wanawake Tunisia

Mamia ya wanaharakati nchini Tunisia wamekuwa wakiandamana kuunga mkono mwanamke anayekabiliwa na mashataka ya utovu wa maadili baada ya kusema alibakwa na polisi.

Maandamano hayo yamefanyika nje ya mahakama mjini Tunis ambapo mwanamke huyo anahojiwa na wachunguzi.

Baadaye wataamua kama watamfikisha mahakamani .

Mwanamke huyo anasema maafisa wawili wa polisi walimsimamisha mwezi uliopita na kumbaka. Maafisa hao wamekanusha madai hayo.

Swala la haki za wanawake limekuwa swala kuu nchini Tunisia wakati muungano unaoongozwa na serikali ya kiislam ukiandaa katiba mpya.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye alidai kubakwa mwezi Septemba akiwa na mpenzi wake wanachunguzwa kwa kile polisi wanachosema ni utovu wa nidhamu hadharani kosa ambalo adhabu yake ni kifungo cha miezi sita gerezani.

Inadaiwa walifumaniwa wakifanya kitendo cha ndoa kwenye gari lao.

Inaarifiwa kuwa polisi waliowafumania walimbaka mwanamke huyo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.