Mtuhumiwa auawa hadharani Mali

Imebadilishwa: 3 Oktoba, 2012 - Saa 08:48 GMT
Wapiganaji wa Kiislamu, Mali

Wapiganaji wa Kiislamu katika eneo la Kaskazini mwa Mali, wamemuuwa Mwanamume mmoja anayetuhumiwa kutekeleza Mauaji.

Kulingana na walioshuhudia, Umati wa zaidi ya watu mia moja ulishuhudia Mtuhumiwa huyo akipigwa risasi na kuuawa na kikosi cha wapiganaji Mjini Timbuktu.

Mwanamume huyo anadaiwa kuwa mwanachama wa kundi la waasi la MNLA kutoka kabila la Tuareg. Kundi hilo lilikuwa na uhusiano wa kirafiki na Wapiganaji wa Kiislamu kabla ya uhasama kuzuka kati yao.

Makundi ya Wapiganaji wa Kiislamu yakijumuisha kundi la Al-Qaeda katika eneo la Maghreb, yalichukua umiliki wa eneo hilo la kaskazini mwa Mali mapema mwaka huu.

Ripoti zinadokeza kuwa mauaji hayo yanayofanywa hadharani ni miongoni mwa hatua za hivi punde zinazoashiria azma ya Wapiganaji hao wa Kiislamu kuanzisha mfumo wa Utawala wa Sharia.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.