Kampuni ya China yamshtaki Obama

Imebadilishwa: 3 Oktoba, 2012 - Saa 10:00 GMT
Rais Barrack Obama

Kampuni moja ya Marekani inayomilikiwa na Uchina imemshtaki Rais Barrack Obama kwa kuizuia kununua mashamba manne.

Mashamba hayo yaliyopo karibu na kambi ya Wanamaji katika eneo la Oregon, yalipangiwa kutumika kuzalisha kawi ya upepo .

Kampuni hiyo, Ralls Corporation, inasema ni kinyume cha sheria na maonevu kwa Obama kutoa uamuzi wa kuizuia kununua mashamba hayo wiki iliyopita kwa sababu za kiusalama.

Kambi hiyo ya Wanamaji inatumika kufanyia majaribio ndege zisizo na marubani.

Shirika la habari la Uchina limesema uamuzi huo wa Obama unahusiana zaidi na Uchaguzi wa Marekani kuliko masuala ya kiusalama.

Hii ni mara ya kwanza kwa Mwekezaji wa kigeni kuekewa kikwazo nchini Marekani katika muda wa miaka 20.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.