Meli yazuiliwa kutokana na madeni

Imebadilishwa: 4 Oktoba, 2012 - Saa 11:29 GMT

Meli ya kifahari

Meli moja ya abiria kutoka nchini Argentina inazuiliwa nchini Ghana kutokana na nchi hiyo kushindwa kulipa madeni inayodaiwa na wawekezaji wake waliopoteza fedha zao mnamo mwaka 2001 .

Meli hiyo iliyokuwa ziarani Afrika, ilizuiwa kuondoka nchini Ghana kufuatia agizo la mahakama.

Kwa upande wake serikali ya Argentina kupitia kwa waziri wake wa mambo ya nje imeshtumu vikali hatua ya kuzuiliwa kwa meli hiyo na kudai kuwa ni njama ya watu wanaotaka kufaidi kiharamu na hivyo kukiuka sheria za kimataifa.

Tayari Argentina imezungumza na taifa hilo ili kubadili hatua hiyo ambayo imechangiwa pakubwa na mzozo kati ya Argentina na wawekezaji wake.

Ombi hili lilifikishwa mahakamani na kampuni moja yenye makao yake Uingereza ijulikanayo kama NML CAPITAL.

Argentina ndiyo nchi ambayo ilikosa kulipa deni kubwa zaidi duniani, dola bilioni miamoja kati ya mwaka 2001-2002. Hata hivyo madeni hayo yalilipwa huku waekezaji wakipata takriban asilimia thelathini na pesa zao zilizopotea.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.