Abu Hamza awasili Marekani

Imebadilishwa: 6 Oktoba, 2012 - Saa 10:01 GMT

Mhubiri wa Kiislamu mwenye msimamo mkali, Abu Hamza, na watu wengine wane wanaoshukiwa kuwa magaida, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumamosi nchini Marekani baada ya kusafirishwa kutoka Uingereza.

Magari ya polisi yakimlinda Abu hamza wakati wa kuondoka UIngereza

Juhudi zao zilizogharimu fedha nyingi, kupinga kupelekwa Marekani, zilimalizika Ijumaa mjini London baada ya mahakama makuu kutupilia mbali rufaa iliyowasilishwa na Bwana Hamza.

Washukiwa hao watano walisafirishwa kwa ndege punde baadaye kuelekea Marekani.

Abu Hamza anakabili mashtaka kadha, pamoja na njama ya kuanzisha kituo cha mafunzo ya kijeshi katika jimbo la Oregon, Marekani.

Yeye na washukiwa wawili watafikishwa mahakama ya New York, na wawili wengine watafanyiwa kesi Connecticut.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.