Libya yazingatia baraza la mawaziri

Imebadilishwa: 7 Oktoba, 2012 - Saa 17:49 GMT

Waziri Mkuu mteule wa Libya, Mustafa Abou-shagour, ametoa wito kuundwe serikali ya dharura katika jaribio lake la pili na la mwisho kuunda baraza lake la mawaziri.

Wananchi wa Libya

Bunge la Libya lenye wajumbe 200 lilikataa orodha ya mawaziri aliyopendekeza mwisho wa juma lilopita, na sasa linazingatia orodha mpya.

Tangazo hilo halikutarajiwa, lakini inaelekea limewapendeza Walibya kwa sababu linafuata matakwa yao.

Waziri Mkuu mteule wa Libya, Mustafa Aboushagour, amependekeza baraza la dharura la mawaziri 10 tu, ikilinganishwa na 29 alilopendekeza juma lililopita.

Alisema hilo ni pendekezo la kuongoza Libya bila ya kufikiria majimbo.

Nchi inakabiliwa na changamoto hatari, alisema Bwana Aboushagour.

Iwapo orodha hiyo mpya piya itakataliwa na bunge, basi waziri mkuu itambidi kujiuzulu.

Baada ya kushindwa mara ya kwanza waziri mkuu alivishauri vyama na akaona kila kimoja kinavutia kwake kwa kudai wizara nyingi.

Bwana Aboushagour amesema hatakubali shinikizo.

Matokeo na yawe vyovyote vile, msimamo wake unaweza kuleta mabadiliko katika siasa changa za Libya.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.