Waziri wa ulinzi mashakani DRC

Imebadilishwa: 10 Oktoba, 2012 - Saa 10:23 GMT

Milipuko ilionekana kutoka upande mmoja wa mto Congo

Waziri wa ulinzi nchini Congo, ameshutumu hatua ya kumfungulia mashtaka ,kuhusiana na milipuko ya zana za vita zilizokuwa katika bohari la silaha mjini Kinshasa mwezi Machi.

Waziri Charles Zacharie Bowao, alisema kuwa mashtaka hayo yameshinikizwa kisiasa kwani serikali inatafuta tu mtu wa kumsingizia mkasa huo.

Takriban watu 240 waliuawa katika mlipuko huo, mjini Brazzaville na wengine zaidi ya 2,300 wakajeruhiwa.

Siku chache baada ya tukio hilo, waziri Bowao, aliutaja mkasa huo kama tukio dogo tu ambalo halikuwa na athari kubwa.

Aliondolewa kwenye baraza la mawaziri mwezi jana wakati wa mabadiliko yaliyofanywa na Rais Joseph Kabila.

Bwana Bowao, alishtakiwa wiki jana, ingawa tangazo hilo halikutolewa hadharani hadi barua aliyoandika kwa chama tawala kuelezea ghadhabu yake ilipofichuliwa.

Anasema anatuhumiwa kwa kutoshughulikia vyema hali iliyosababisha kulipuka kwa silaha hizo na inaarifiwa kuwa anajiandaa kukata rufaa.

Milipuko hiyo iliyosemekana kusababishwa na hitilafu ya mitambo ya umeme, ilikuwa mikubwa kiasi cha kuvunja madirisha na paa za bohari hilo.

Watu wengine 26 wengi wakiwa maafisa wa jeshi, wameshtakiwa kuhusiana na milipuko hiyo na wangali wanazuiliwa wakisubiri kufunguliwa mashtaka.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.