Uchunguzi wa madawa bandia ya ARV Tanzania

Imebadilishwa: 12 Oktoba, 2012 - Saa 10:14 GMT

Madawa bandia ya ARV

Uchunguzi unaoendelea kuhusu kusambazwa kwa madawa bandia ya kukabiliana na makali ya virusi vya HIV, nchini Tanzania huenda ukasababisha kufunguliwa kwa kesi za uhalifu

Waziri wa afya Tanzania,Dr Hussein Mwinyi amewafuta kazi kwa muda maafisa wakuu watatu na kusitisha uzalishaji wa dawa hizo nchini humo wakati uchunguzi ukiendelea.

Aliambia BBC kuwa hataruhusu watu kuhujumu maisha ya watanzania. Bwana Mwinyi, alisema kuwa polisi na maafisa wengine wa usalama wanahusika na uchunguzi huo.

Wadadisi wanasema kuwa kuna wasiwasi kuhusu ubora wa madawa yanayozalishwa nchini humo, hasa ikizingatiwa visa vingi vya ufisadi, katika nyanja za kisiasa nchini humo.

Mapema mwaka huu, tume inayotathmini matumizi ya pesa za serikali, ilifichua matumizi mabaya ya pesa za umma, ikiwemo katika wizara ya afya. Kashfa hiyo ilisababisha kufutwa kazi kwa mawaziri saba wa serikali.

Dr Mwinyi alisema kuwa wizara ya afya ilitahadharishwa mnamo mwezi Agosti, kuhusu matatizo ya namba za usajili kwenye baadhi ya madawa ya ARV katika hospitali ya wilaya ya Tarime.

Maafisa watatu waliofutwa kazi kwa muda wanafanya kazi katika idara ya kuhifadhi madawa na sasa uzalishaji wote wa madawa hao umesitishwa.

Wagonjwa wa HIV hupokea matibabu ya bure Tanzania. Waziri alisema kuwa kati ya chupa 12,000 za madawa, chupa 9,570 ziliondolewa madukani .

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.