Wanawake kurithi Mali Botswana

Imebadilishwa: 12 Oktoba, 2012 - Saa 13:50 GMT

Wanawake wamekuwa wakinyimwa nafasi ya kurithi Botswana

Mahakama kuu nchini Botswana imebatilisha sheria ya kitamaduni ambayo iliwazuia wanawake kurithi mali nyumbani.

Mahakama imesema kuwa kanuni hiyo ya kitamaduni inakiuka sheria ya katiba inayosisitiza usawa kwa wanaume na wanawake.

Edith Mmusi na dadake zake watatu walilazimika kwenda mahakamani baada ya mpwa wao kusema kuwa yeye ndiye mmiliki wa nyumba yao.

Duru zinasema kuwa wanawake hawaruhusiwi kurithi mali katika jamii nyingi za kiafrika ingawa katika baadhi ya nchi sheria hizo sasa zinaharamishwa.

Mwandishi wa BBC mjini Gaborone, anasema kuwa uamuzi wa jaji Key Dingake, sasa inaileta katika safu moja sheria ya utamaduni na katiba ya nchi.

Alisema kuwa lazima pawepo usawa kati ya wanawake na wanaume kuhusiana na swala urithi.

Mmoja wa madada hao waliofika katika mahakama kupinga sheria za kitamaduni , alijawa na furaha isiyo na kifani.

"ni siku nzuri sana kwetu'' alisema bi Mmusi

Uamuzi wa leo unafikisha kileleni kesi ambayo imekuwa ikiendelea kwa miaka mitano ambayo yeye na madada zake walifikisha mahakamani.

Mussi walienda mwanzo katika mahakama za kitamaduni kupinga hatua ya mpwa wao mnamo mwaka 2007.

Lakini walishindwa katika kesi hiyo mara mbili ndiposa wakaamua kwenda katika mahakama ya kiraia.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.