Wakamatwa kwa vurugu za kidini Tanzania

Imebadilishwa: 16 Oktoba, 2012 - Saa 09:50 GMT

Maandamano ya kidini Tanzania

Polisi nchini Tanzania wamewakamata watu 126 baada ya mashambulizi ya wiki jana dhidi ya makanisa mjini Dar es Salaam kwa mujibu wa kamanda wa polisi.

Waisilamu waliokuwa wameghadhabishwa walivunja na kuharibu makanisa matano baada ya kijana mmoja kuripotiwa kuikojolea Quran

Rais Jakaya Kikwete , alisema kuwa ghasia hizo hazikubaliki hata kama kitendo kama hicho kimefanyika na kuwaghadhabisha waisilamu.

Historia ndefu ya watu kuvumiliana kidini haipaswi kupuuzwa, alisema Rais Kikwete.

Mwandishi wa BBC Aboubakar Famau mjini Dar es Salaam anasema kuwa ubishi ulitokea kati ya kijana mwenye umri wa miaka 14 mkristo na rafiki yake musilamu, hali iliyosababisha matukio ya vurugu siku ya Ijumaa.

'Haki itendeke'

Ubishi ulitokea baada ya kijana huyo mkristo kuambiwa na mwenzake muisilamu kuwa angebadilika na kuwa nyoka ikiwa angeikojolea Quran.

Na kijana huyo akaitisha kitabu hicho na kisha kukikjolea ili kuona kama kweli madai ya mwenzake yangetokea.

Kamanda mkuu wa polisi mjini Dar es Salama, Suleiman Kova, aliambia BBC kuwa watu 126 wamekamawa kuhusiana na tukio hilo.

Mhubiri wa kiisilamu Sheikh Alhadi Musa, ambaye ni mwenyekiti wa kamati moja ya kidini, alilaani mashambulizi hayo dhidi ya makanisa

Alisema kuwa kuwa Quran imekejeliwa na mtu mmoja kwa hivyo sio sawa kuchukulia hatua hiyo kama msimamo wa wakristo wote.

Mipango inafanyika ya mikakati ya amani kufanyika kati ya waumini wa dini hizo mbili.

Rais Kikwete aliyetembelea makanisa yaliyoshambuliwa siku ya Jumamosi alitoa wito wa amani na kusema kuwa wakristo hawapaswi kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi kwani hatua hiyo itachochea vurugu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.