Jeshi la Somalia ladaiwa kupora watu

Imebadilishwa: 16 Oktoba, 2012 - Saa 10:37 GMT

Wanajeshi wa Somalia

Wenyeji wa mji wa Kismayo, nchini Somalia wanasema kuwa kumetokea visa vya uporaji vilivyofanywa na wanajeshi wa serikali ya Somalia.

Mapema mwezi huu, wanajeshi wa Somalia kwa ushirikiano na vikosi vya Muungano wa Afrika, walidhibiti mji huo ambao ulikuwa umetekwa na wanamgmbo wa Al Shabab.

Wenyeji wameambia BBC kuwa wanajeshi wa Somalia wanavamia nyumba za watu na kuiba pesa na simu za mkononi.

Hata hivyo serikali ya Somalia haijasema lolote kuhusiana na madai hayo.

Awali kulikuwa na tuhuma kama hizi dhidi ya jeshi hilo,wakati walipotwaa udhibiti wa mji mwingine wa Somalia wa Afgoye mnamo mwezi Mei.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.