Naibu jaji mkuu wa Kenya ajiuzulu

Imebadilishwa: 18 Oktoba, 2012 - Saa 14:34 GMT

Aliyekuwa naibu jaji mkuu wa Kenya Nancy Baraza

Naibu jaji mkuu wa Kenya Nancy Baraza amejizulu baada ya jopo la majaji kutaka aachie ngazi kufutia madai ya kutishia maisha ya mlinzi mmoja kwa banduki katika duka moja la kifahara mjini Nairobi

Nancy Baraza alisema kuwa alihisi haki isingetendeka ikiwa engekata rufaa dhidi ya uamuzi wa jopo la majaji maalum waliosikiza kesi dhidi yake na kupeleka kesi yake katika mahakama ya juu zaidi nchini.

Aliongeza kuwa jaji mkuu wa Kenya Willy Mutunga ambaye ni rais wa mahakama ya juu zaidi, alipitisha mapendekezo ya jopo hilo la majaji katika mahojiano kwenye televisheni na kwa hivyo asingetoa uamuzi wa haki kwenye kesi yake ya rufaa.

Aidha ameelezea kuwa majaji wengine wawili katika mahakama hiyo walipendekeza kuwa jopo liundwe ili kuchunguza madai dhidi yake.

Jopo la majaji saba likiongozwa na aliyekuwa jaji mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhani, ilimpata Baraza na hatia ya kutishia maisha ya mlinzi Rebecca Kerubo, katika duka la kifahari la Village Market alipotaka kupekua kibeti chake kabla ya kuingia kwenye duka hilo.

Ulinzi nchini Kenya umedhibitiwa sana hasa baada ya jeshi la Kenya kwenda Somalia kupambana na Al Shabaab. Na kila sehemu ya maduka walinzi hupekua mizigo ya watu kama tahadhari tu ya kuhakikisha usalama wa watu.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.