Kiongozi wa kiisilamu atoweka Zanzibar

Imebadilishwa: 18 Oktoba, 2012 - Saa 08:40 GMT

Ramani ya Zanzibar

Wasiwasi umetanda kisiwani Zanzibar kufuatia kutoweka kwa kiongozi wa kidini Sheikh Farid Hadi Ahmed.

Watu wawili wametiwa nguvuni waliohusika na maandamano na ghasia zilizosababisha uharibifu mkubwa kisiwani humo.

Kuna hofu kuwa kiongozi huyo huenda amekamatwa na polisi na anazuiliwa Tanzania bara kutokana na kuwa amepinga utawala wa chama tawala cha Tanzania bara CCM.

Kwingineko, hapo jana polisi nchini Tanzania walimkamata mhubiri mwenye utata anayetuhumiwa kwa kuchochea vurugu wiki jana , na kusababisha maandamano mapya.

Kulingana mkuu wa polisi, Suleiman Kova ,Sheikh Ponda Issa Ponda, mkuu wa Jumuiya ya waislamu, vuguvugu ambalo halitambuliki na serikali ya Tanzania, alikamatwa kwa kuchochea vurugu.

Kukamatwa kwa Sheikh Ponda, mini Dar es Salaam, inakuja baada ya kukamatwa kwa watu 31 waliozua vurugu na kupora mali ya watu wakati waandamanaji walijawa na ghadhabu na kuandamana wiki jana wakiharibu makanisa kadhaa mjini humo.

Maandamano ya wiki jana yalisababishwa na tetesi kuwa kijana mwenye umri wa miaka kumi na miwili aliikojolea Quran.

Ponda amekuwa akiwaongoza wafuasi wake kufanya maandamano kinyume na sheria na kutoa wito wa ghasia na umwagikaji damu mjini Dar es Salaam na nchini kote.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.