Wakuu wa migodi kutopokea mishahara

Imebadilishwa: 18 Oktoba, 2012 - Saa 09:19 GMT

Vurugu migodini Afrika Kusini

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, amewataka wafanyakazi wa migodini kurejea kazini baada ya migomo iliyokumbwa na ghasia.

Baada ya mkutano wa masaa tano na viongozi wa vyama vya wafanyakazi, bwana Zuma alitoa wito wa kutaka uzalishaji wa madini migodini kurejealea hali yake ya kawaida.

Zuma pia amewataka vwafanyabiashara wakuu nchini humo kutojilipa mishahara angalau kwa mwaka mmoja.

Uzalishaji wa madini nchini Afrika Kusini, umekumbwa na migomo mingi ambayo ilisababisha mauaji ya wachimba migodi zaidi ya arobaini.

Kampuni ya madini ya Anglo American Platinum wiki jana iliwafuta kazi wachimba migodi 12,000 waliokuwa wanagoma.

Kampuni ya Amplat ndiyo mojawapo ya makampuni makubwa ya kuchimba madini duniani.

Wachimba migodi 15,000 katika mgodi wa Gold Fields, ambayo ni ya nne kwa ukubwa zaidi kuzalisha dhahabu duniani, huenda wakafutwa kazi ikiwa hawatarejea kazini saa nane mchana wa leo.

"Tukubaliane kuanzia sasa kuwa lazima ghasia zikome. Ghasia hazina nafasi katika mfumo wetu na pia zina athari kubwa kwa kazi zetu'' alisema bwana Zuma

Pia aliwataka wakurugenzi wakuu kusimamisha mishahara yao na marupurupu yao ya mwaka ujao ili wachangie katika kujenga nchi yenye uchumi thabiti.

Kauli ya Zuma ndiyo ya kwanza nzito tangu kuanza kwa vurugu migodini.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.