Mkutano mkuu kuhusu Tuareg nchini Mali

Imebadilishwa: 19 Oktoba, 2012 - Saa 15:15 GMT

Rais wa mpito nchini Mali Dioncounda Traore anataka wanajeshi kupelekwa nchini mwake

Viongozi wa dunia wanakutana katika mji mkuu Bamako nchini Mali kujadili mgogoro wa eneo la Kaskazini nchini humo lililonyakuliwa na vikosi vya wapiganaji wa kiislamu.

Mkuu mpya wa Umoja wa Afrika Nkosozana Dlamini-Zuma aliyeko mjini Bamako amesema utatuzi wa mgogoro huo ni moja ya mambo muhimu ya kipaumbele kwake.

Rais wa mpito nchini Mali Dioncounda Traore amesema anataka wanajeshi kupelekwa nchini mwake ili kukabiliana na wapiganaji wa Tuareg.

Wiki iliyopita Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilipitisha azimio linalotoa mwanya wa uvamizi wa kijeshi kaskazini mwa Mali.

Yacouba Kone, meneja wa shirika la misaada nchini humo la Christian Aid, ameiambia BBC kuwa hali ya kibinadamu nchini humo imo hatarini.

Katika mkutano uliofanyika wiki jana mjini Brussels,Muungano wa Ulaya ulisema kuwa hali nchini Mali ni tisho kwa Ulaya.

Aidha baraza la usalama la umoja huo ilipitisha azimio ambalo liliruhusu harakati za jeshi kuzima uasi Kaskazini mwa Mali.

Shirika la kikanda la Ecowas lilipewa siku arobaini na tano kuelezea mpango wake wa kutuma wanajeshi 3,000 katika eneo hilo.

Wapiganaji wa Tuareg Kaskazini mwa Mali

Ufaransa iko tayari kuingilia kati mzozo huo ingawa nchi zingine bado hazijaelezea nia hiyo.

Waakilishi kutoka nchi 20 , mashirika kadhaa ya kimataifa na maafisa wakuu akiwemo mjumbe maalum wa umoja wa mataifa katika eneo hilo Romano Prodi, wanahudhuria mkutano huo.

Baada ya mkutano wa Brussels, viongozi wa Muungano wa Ulaya walisema kwa kauli moja kuwa hali nchini Mali ni tisho kwa usalama kwa eneo zima la Sahel pamoja na nchi za Magharibi mwa Afrika, Afrika Kaskazini na Ulaya.

Kundi la wapiganaji wa kiisilamu wa Tuareg, walidhibiti eneo la Kaskazini mwa Mali baada ya mapinduzi ya kijeshi mwezi Machi

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.