Sudan.K kuanza tena kuzalisha mafuta

Imebadilishwa: 19 Oktoba, 2012 - Saa 08:40 GMT

Shughuli za kuzalisha mafuta kuanza tena Sudan Kusini

Sudan Kusini imeamuru makampuni ya mafuta kuanza kuzalisha mafuta mara moja.

Hatua hii inamaliza mgogoro wa mafuta kati ya nchi hiyo na Khartoum.

Nchi hiyo ilisitisha uzalishaji wa mafuta mwezi Januari katika mzozo kuhusu deni lake kwa Khartoum kwa kusafirishia mafuta kupitia kwa mabomba yake.

Hali ya taharuki kati ya nchi hizo nusuru izitumbukize katika vita.

Makubaliano yaliafikiwa mwezi jana ya kusuluhisha mzozo na kupitishwa na bunge la Sudan.

Waziri wa mafuta wa Sudan Kusini, alisema kuwa itachukua miezi mitatu kabla ya mafuta ya nchi hiyo kufikia soko la kimataifa.

Sudan Kusini ilijitangazia uhuru wake mwezi Julai mwaka jana na kuchukua thuluthi mbili ya rasilimali za mafuta za Sudan ingawa Sudan ikasalia na vifaa vya kusafisha mafuta pamoja na kuyasafirisha.

Uhusiano kati ya nchi hizo ulizorota sio kwa sababu ya mafuta tu bali pia kuhusu mpaka wa nchi hizo swala ambalo hadi sasa bado halijapata ufumbuzi.

Uchumi wa nchi hizo, umeathirika sana kwa sababu ya hatua ya kusitisha usafirishaji wa mafuta hayo kutoka sudan Kusini na hivyo kusababisha hasara ya asilimia 98 kwa uchumi wa nchi hiyo.

Mwishoni mwa mwezi jana, viongozi wa Sudan na Sudan Kusini, walikubaliana kuanza tena kuuza mafuta lakini maelezo machache sana yameweza kutolewa kuhusu mkataba uliofikiwa kwa usaidizi wa Muungano wa Afrika.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.