Aliyekuwa kiongozi wa Misri achunguzwa

Imebadilishwa: 21 Oktoba, 2012 - Saa 15:35 GMT

Wakuu wa Misri wanasema kuwa wamezuwia mali ya waziri mkuu wa mwisho wa utawala wa Rais Hosni Mubarak.

Bwana Ahmed Shafiq wakati wa kampeni za uchaguzi wa rais mwezi Juni

Mwanasiasa huyo ni Ahmed Shafiq ambaye alishindwa kwa kura chache na Mohammed Morsi kwenye uchaguzi wa rais mwezi wa Juni.

Msemaji wa wizara ya sheria ya Misri alisema kuwa wanachunguza tuhuma kwamba Bwana Shafiq alipata mali yake nyingi kwa njia zisokuwa halali, pamoja na nyumba 12 na fleti mbili.

Bwana Shafiq, ambaye hivi sasa yuko katika Falme za Kiarabu, amekanusha tuhuma hizo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.