Boko Haram waua wanajeshi Potiskum

Imebadilishwa: 22 Oktoba, 2012 - Saa 15:02 GMT

Mashambulizi yaliyofanywa na Boko Haram mjini Potiskum


Wanajeshi kadhaa wameuawa na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram Kaskazini Mashariki mwa mji wa Potiskum.

Mji wa Potiskum umeshuhudia siku kadhaa za mapigano na watu 31 wakiuawa na wengine wengi kujeruhiwa pamoja na mamia kadhaa kutoroka mji hu.

Wakati huohuo, China imeelezea kero lake kuhusu mauaji ya mfanyakazi mmoja wa kichina Kaskazini Mashariki mwa mji wa Maiduguri.

Boko Haram wanatetea kile wanachosema ni kuitaka serikali ya Nigeria kutumia sheria za kiisilamu.

Mnamo siku ya Ijumaa, jeshi lilisema kuwa lilimkamata kamanda mkuu wa kundi hilo, Shuaibu Muhammed Bama, akiwa katika makaazi ya seneta mmoja mjini Maiduguri, ambako Boko Haram walianzia harakati zao.

Madai hayo yameanzisha fununu kuwa huenda wanasiasa wanawasaidia wapiganaji hao.

Mwandishi wa BBC nchini Nigeria Will Ross, amedokeza kuwa mgogoro unaokumba mji wa Potiskum umefikia viwango vya juu ambapo sasa visa vya ufyatulianaji wa risasi, mashambulizi ya mabomu na mauaji ya kupangwa vimekithiri

Katika ghasia za hivi karibuni,washukiwa Boko Haram waliwashambulia kwa mabomu wanajeshi.

''Baadhi ya wanajeshi wetu waliuawa lakini sheria ni kuwa familia zao lazima zijulishwe mwanzo, kabloa ya kutangaza kwa mtu yeyote,'' alisema kamanda wa majeshi

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.