Mashambulizi ya maguruneti Kismayo

Imebadilishwa: 22 Oktoba, 2012 - Saa 14:56 GMT

Wanajeshi wa AU mjini Kismayo

Mashambulizi mawili ya guruneti yametokea mjini Kismayo , mji ambao hivi karibuni ulikombolewa na wanajeshi wa Muungano wa Afrika.

Kambi ya wanajeshi wa Somalia ndiyo ililengwa kwa mashambulizi hayo.

Mwandishi wa BBC mjini Mogadishu anasema kuwa haya ndiyo mashambulizi ya kwanza kutokea mjini humo tangu wanamgambo wa Al Shabaab kufurushwa kutoka mjini humo mapema mwezi huu.

Anasema kuwa ni dalili ya mambo yatakavyokuwa katika siku za usoni hasa baada ya Al Shabaab kusema itafanya mashambulizi ya kuvizia pamoja na ya kujitoa mhanga kufuatia kufurushwa kwao.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.