Mafuta yanayoibwa Nigeria huishia ulaya

Imebadilishwa: 23 Oktoba, 2012 - Saa 11:57 GMT

Eneo la Niger Delta ndilo linazalisha mafuta mengi ya Nigeria

Wateja wakubwa wa mapipa laki mia moja na themanini ya mafuta yanayoibwa kutoka nchini Nigeria wako katika nchi za Kusini Mashariki mwa Ulaya pamoja na Singapore, kulingana na wanaharakati.

Mwanasiasa kutoka jimbo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta, Patrick Dele Cole, amesema kuwa asilimia tisini ya mafuta yanayoibwa yanasafirishwa kwenda nje ya nchi kinyume na sheria.

Amezindua kampeini yenye kauli mbiu ''Komesha wizi'' ili kumaliza visa vya wizi wa mafuta.

Nigeria ni mojawapo ya nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi ingawa idadi kubwa ya wananchi wake wanaishi kwa umaskini

Kampeini hiyo inalenga kuzichunguza meli hizo kwa satelite na kubaini pesa zinazotokana na uuzaji huo zinakokwenda.

''Unapoanza kuuliza maswali, na kuanza kuangazia swala hili, utakuwa umesuluhisha zaidi ya asilimia hamsini ya matatizo kuhusiana na wizi wa mafuta.'' alisema bwana Dele Cole, mwanadiplomasia mkongwe na mshauri wa zamani wa rais.

''Nadhani ni mumimu kutoa onyo kwa wale matajiri kwamba siku yao ya kuwajibika itafika''

Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa sekta nzima ya mafuta nchini humo inakumbwa na ufisadi,

Wanasiasa wengi wanahusika na wizi huo anasema Will, huku sehemu ya mapato ya mafuta hayo yakitumiwa kununua kura na kufadhili kampeini zao.

Jeshi la Nigeria linapaswa kusitisha visa vya wizi wa mafuta lakini wao huchukua hongo ili kutofuatialia visa hivyo

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.