Wakulima wa Afrika wapunguziwe Vikwazo

Imebadilishwa: 25 Oktoba, 2012 - Saa 07:55 GMT

Uhaba wa chakula Afrika ni tatizo kubwa

Ripoti ya Benki ya dunia kuhusu chakula barani Afrika inasema kuwa wakulima wanaweza tu kuzalisha chakula cha kutosha kulisha watu wa bara hilo ikiwa vikwazo vya biashara kati ya nchi hizo vitapunguzwa.

Mamilioni ya watu katika eneo la Sahel wanakumbwa na njaa na utapia mlo.

Kwa mujibu wa benki hiyo, tatizo la uhaba wa chakula litapunguka tu ikiwa wakulima katika maeneo yenye kuzalisha chakua wataweza kuruhusiwa kusafirisha mazoa yao kupitia mipaka bila malipo.

Kuondoa vikwazo vya mipakani, pia itapunguza gharama ya chakula.

Benki ya dunia inasema kuwa asilimia tano ya nafaka barani Afrika inatoka katika mataifa mengine ya Afrika ikisema kuwa mashamba makubwa yenye dhoruba hayatumiwi kwa upanzi.

Je hii ndio sababu ya uhaba wa chakula Afrika kweli? Toa maoni yako kwenye ukurasa wetu wa Facebook bbcswahili

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.