Gbagbo akataliwa kuachiwa kwa dhamana

Imebadilishwa: 27 Oktoba, 2012 - Saa 15:50 GMT
Gbagbo akiwa ICC

Mahakama ya jinai ya kimataifa mjini Hague, ICC, imekataa rufaa ya rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, kwamba aachiliwe kwa dhamana kabla ya kesi yake kuanza.

Jaji kwenye kesi hiyo, Sanji Monagan, alisema mahakama yametenda haki:

"Mahakama ya rufaa inaona kuwa katika hali hii, uamuzi wowote katika mahakama ya kabla ya kesi, kuhusu Bwana Gbagbo kuendelea na kifungo au kuachiliwa kwa sababu ya afya yake, utakuwa umechukuliwa mapema mno.

Kwa hivo mahakama ya rufaa inaona kuwa mahakama yaliyotangulia kesi hayakukosa kwa kutozingatia afya ya Bwana Gbagbo katika hali ya sasa."

Bwana Gbagbo anakabili mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu wakati wa ghasia zilizofuatia uchaguzi miaka miwili iliyopita.

Watu zaidi ya 3000 waliuwawa na malaki walihama makwao, baada ya Bwana Gbagbo kukataa kwamba alishindwa kwenye uchaguzi.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.