Wachimba migodi warudishwa kazini

Imebadilishwa: 27 Oktoba, 2012 - Saa 11:43 GMT

Kampuni inayochimba dhahabu nyeupe nyingi kabisa duniani, Anglo American Platinum, imekubali kuwarejesha makazini wachimba migodi 12,000 wa Afrika Kusini iliowatoa kwa sababu waligoma kinyume cha sheria.

Wachimba migodi waliokuwa wakigoma wa Anglo American

Chama cha wachimba migodi, NUM, kimesema kuwa kampuni hiyo imekubali kuwapokea wachimba migodi iwapo watarudi makazini Jumaane.

Sekta ya migodi ya Afrika Kusin imekumbwa na migomo kadha ambayo serikali inasema imegharimu nchi zaidi ya dola bilioni moja.

Watu kadha wameuwawa kwenye ghasia zilizohusu migomo hiyo.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.