Idadi ya watu A. Kusini yaongezeka

Imebadilishwa: 30 Oktoba, 2012 - Saa 10:02 GMT

Ripoti ya idadi ya watu nchini Afrika Kusini imetolewa.

Ripoti hiyo inaonyesha idadi ya watu imeongezeka kwa watu milioni saba katika mwongo mmoja uliopita.

Nchi hiyo sasa ina takriban watu milioni hamsini na mbili lakini licha ya licha kumaliza kwa enzi ya ubaguzi wa rangi ingali imegawanyika katika misingi hiyo.

Familia nyingi za kiafrika zimeshuhudia mapato yao yakipanda kwa kasi kuliko kundi lengine lolote la watu, lakini wazungu wangali wanapata mara sita ya waafrika weusi.

Takriban watu milioni mbili wangali wanaishi katika mitaa ya mabanda, idadi yao ikipanda kwa zaidi ya watu laki moja tangu mwaka 2001.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.