Washukiwa wa ugaidi wanaswa Morocco

Imebadilishwa: 2 Novemba, 2012 - Saa 11:18 GMT
Shambulio la Kigaidi Morocco

Shambulio la Kigaidi Morocco

Serikali ya Morocco, imesema kuwa imesambaratisha kundi moja la kigaidi ambalo lilikuwa likijaribu kuanzisha kambi ya mafunzo katika milima ya Rif.

Wizara ya mambo ya ndani nchini humo, imesema maafisa wa polisi wamewakamata washukiwa tisa na kunasa vifaa kadhaa, vikiwa ni pamoja na bendera nyeusi inayotumiwa na kundi la kigaidi la Al-Qaeda.

Washukiwa hao walikamatwa baada ya polisi kupata habari zao kutoka kwa washukiwa wengine wawili waliokamatwa mwezi uliopita mjini Rabat.

Siku ya Jumatano wiki hiyo, maafisa wa polisi nchini Ujerumani, walimkamata raia mmoja wa Ufaransa anayesakwa na serikali ya Morocco kuhusiana na mashambulio ya mambomu mwaka wa 2003.

Watu 45, waliuawa kwenye mashambulio hayo yaliyotekelezwa katika mji mkuu wa Morocco, Casablanca.

Kwa Mujibu wa taarifa kutoka kwa wizara ya mambo ya ndani,watano kati ya washukiwa hao wamewekwa rumande na wengine wanne wanazuiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.

Taarifa hiyo imesema, uchunguzi umebainisha kuwa, washukiwa hao walikuwa na njama ya kuanzisha kambi ya kutoka mafunzo kwa wanajeshi wa waasi, katika milima ya Rif, kinyume na sheria za nchi hiyo.

Ripoti zinasema wanachama wa kundi hilo walipanga kuunda vilipuzi na kushambulia majengo ya kibiashara yanayouzwa ili kufadhili shughuli zao.

Wizara hiyo ya mambo ya ndani imesema kundi hilo, lilikuwa limeweka kituo bandi cha ukaguzi mjini Ouazzane.

Mwezi Aprili mwaka huu, watu 17, waliuawa kwenye shambulio la bomu, katika mgahawa mmoja mjini Marrakech.

Hata hivyo kundi la kigaidi ya Al-Qaeda katika eneo la Kaskazini mwa Afrika, lilikanusha kuhusika na shambulio hilo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.